Tuesday, 7 July 2015

Watuhumiwa 133 wa mauwaji ya Albino watiwa mbaroni

Watuhumiwa 133 wa mauaji ya watu wenye ualbino wamefanikiwa kukamatwa nchini huku watuhumiwa 14 wamepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Akizungumza na vyombo ha habari jijini Dar es Salaam waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe, amesema katika kipindi cha miaka kumi ya serikali ya awamu ya nne, wizara yake imefanikiwa kudhibiti mtandao wa ushirikina na mauaji ya watu wenye ualbino nchini na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 133 na kesi 41 zimefunguliwa ambapo 4 zimekamilika na hadi sasa watuhumiwa 14 wamepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifo huku kesi nyingine ziko katika hatua mbalimbali.
 
Mbali na mafanikio mengine mengi, wizara hiyo imefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhalifu nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola

No comments: