Monday 27 July 2015

Yanga yaongeza nguvu kumsajili Michael Olunga

Yanga yaongeza nguvu kumsajili Michael OlungaMbali na Olunga Yanga pia wanamwania kiungo wa mabingwa hao wa Kenya Khalid Auch, ili kuimarisha safu yao ya kiungo mkabaji
KLABU ya Yanga imeongeza nguvu za kumsajili mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya Michael Olunga, ili kuziba nafasi ya Mliberia Kpah Sherman, anayetarajiwa kujiunga na timu ya Mpumalanga Black Aces inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
Uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu wake Mkuu Dr Joans Tiboroha amesema wanatarajia kuanza mazungumzo na viongozi wa Gor kuangalia uwezekano wa kumpata mshambuliaji huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwnenye michuano ya Kgame inayoendelea Dar es Salaam Tanzania.
“Olunga ni mchezaji mzuri kila mtu analijua hilo na kwakua Sherman wakati wowote ataondoka tumeona yeye ndiyo mtu sahihi wa kuziba nafasi yake kwenye kikosi chetu kusaidiana na Donald Ngoma Amissi Tambwe na Malimi Busungu,”amesema Tiboroha.
Mbali na Olunga Yanga pia wanamwania kiungo wa mabingwa hao wa Kenya Khalid Auch, ili kuimarisha safu yao ya kiungo mkabaji baada ya Mbuyu Twite kuonekana kuchoka kutokana na umri mkubwa aliokuwa nao huku pia klabu yake ya zamani FC Lupopo kuonekana kuisumbua Yanga kutokana na usajili wake.

No comments: