Thursday 2 July 2015

Watu watano na askari mmoja wauawa nchini Burundi

Watu watano wauawa katika mapigano Burundi"Wahalifu" watano na askari mmoja wauawa katika mapigano jijini Bujumbura

Afisa mmoja wa Polisi jijini Bujumbura aliliambia shirika la habari la AFP la Ufaransa kuwa wahalifu watano waliuawa katika mapigano katika wilaya ya Cibitoke jijini Bujumbura.
Cibitoki ni moja ya wilaya ambazo zinatambulika kwa kukipinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza tangu kuanzishwe maandamano nchini Burundi.
Mapigano hayo yametokea Jumatano Julai mosi ikiwa nchi ya Burundi ikiazimisha miaka 53 tangu kujipatia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji.

Taarifa zinafahamisha kuwa mapigano yalitokea baada ya askari Polisi kutupiwa maguruneti matatu na kuwajeruhi askari wawili.

No comments: