Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Gosbert Blandes akiwasilisha
maoni ya kamati hiyo bungeni mjini Dodoma amesema jambo hilo linaweza
kuathiri utekelezaji wa sheria hiyo kwani watumishi waliopo katika
taasisi hizo watakuwa na hofu ya kutoa taarifa za uhalifu dhidi ya wakuu
wao wa kazi hasa pale zitakapokuwa zinawagusa.
Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni katika wizara hiyo Mh
Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya kambi hiyo amesema kambi imependekeza
bunge liwe na mamlaka ya kiuchunguzi katika muswada huo kama sehemu ya
utekelezaji wa mamlaka yake ya kuisimamia serikali chini ya ibara ya 63
kifungu kidogo cha pili ya katiba ya nchi.
Akiwasilisha muswada huo bungeni waziri wa katiba na sheria Dk
Asharoze Miigiro amesema vitendo vinavyoweza kutolewa taarifa kwenye
mamlaka husika ni pamoja na makosa ya jinai au uvunjwaji wa sheria,
vitendo vinavyoathiri afya au usalama wa mtu binafsi au jamii,
ubadhilifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na uharibifu wa
mazingira.
Baadhi ya wabunge wakichangia muswada huo wametaka adhabu kwa
wavujisha siri za watoa taarifa iongezwe, watoa taarifa sahihi
zitakazowezesha ama kuzuia uhalifu uliokuwa ufanyike au kuokoa hasara
ambayo taifa ilikuwaipate wapewe motisha pamoja na kuwapa ulinzi watoa
taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment