Mbunge
mmoja nchini Zimbabwe alizua kizaazaa bungeni pale alitumia chupi za
kina mama kusisitiza hatma ya raia masikini wa nchini hiyo ambao hawana
uwezo wa kununua chupi mpya.
Katika kikao kilichokua kikipeperusha
moja kwa moja kwenye runinga ya taifa, Priscilla Misihairabwi-Mushonga,
wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), alitoa
karatasi ya plastiki iliyokuwa na chupi hiyo. Kisha akamuuliza waziri wa
fedha na sera za serikali kuhusiana na uagizwaji wa chupi kukuu ambayo
anasema ni ya bei nafuu na zinasababisha madhara makubwa kwa afya ya
kina mama.''Bwana spika hebu tazama hizi chupi ninazo hapa, hizi ni mpya na hugharimu dola mbili kila moja.''
Akijibu swali hilo waziri wa fedha Patrick Chinamasa alimtania mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga kutokana na uamuzi wake wa kubeba chupi hizo bungeni lakini amesema wizara yake inachunguza suala hilo. ''Bwana Spika, kabla sijajibu swahili hilo, naamini mheshimiwa mbunge hangelifanya kitendo kama hicho kusisitiza hoja yake'' alisema waziri huyo wa fedha.
Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikali mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF ambaye alimshutumu kwa kutumia matamshi ya kibaguzi.
Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa muda wa miaka kadhaa iliyopita hali iliyosababisha viwango vya umasikini kupanda kutokana na idadi kubwa ya watu wasio na ajira.
Nguo zingine hutengenezwa uchina huku zingine zikitoka Ulaya kama misaada.
Mwaka wa 2012 waziri wa fedha Tendai Biti alitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku uuagizaji wa chupi za mitumba akisema ni tishio kubwa kwa afya ya raia wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment