Viongozi wa Vyama vinavyunda Umoja wa vyama vya Upinzani Tanzania (UKAWA) wakiwa katika Ofisi za Makao makuu ya Chama cha CUF, katika Mkutano na waandishi wa Habari mapema leo. |
Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mwenyekiti
mwenza, ndugu James Mbatia ndie alikuwa wa kwanza kuongea. Ni rai ya
UKAWA kwa kila mtanzania ambae yuko tayari kuondoa mfumo kandamizi wa
CCM kuungana nasi. Tunachukua fursa hii kumualika waziri mkuu mstaafu na
mbunge wa Monduli kujiunga na UKAWA. Ni mchapakazi makini na
mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali
kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki
Tanzania, Mungu ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.
MASWALI
Mnamualika au mnamkaribisha
Vyama vilikuwa vinasema Lowassa ni dhaifu, leo amekua Imara?
Mnamkaribisha kuingia chama gani maana UKAWA ina vayama vingi?
Akikubali kujiunga na nyinyi leo hii mtakubali agombee nafasi ya urais?
Lini mtamtambulisha mgombea wenu urais?
MAJIBU:
Lipumba: Maswali ya ufisadi katika Tanzania ni maswala ya Mfumo, mfumo wa siasa ndio unaoendeleza ufisadi, Lowassa ameachia madaraka mwaka 2008, katika kipindi hiki ufisadi umeongezeka au yamepungua? Pia yeye mwenyewe alisema mwenye ushahidi aende mahakamani.
Swala la kumtangaza mgombea urais ni utaratibu wa vyama,Lakini nina uhakika Mwanzoni mwa mwezi August tutakuwa tumepata mgombea urais ambae atapeperusha bendera ya UKAWA.
Kuhusu Lowassa kuepewa nafasi ya kugombea urais: Hilo ni swala la mchakato, mgombea urais atapatika kwa utaratibu ambao upo kikatiba.
Mzee Makaidi (NLD)
Lowassa ni mtu safi hadi pale atakapobainika mahakamani ni mchafu.
Mbatia
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake. Watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi. Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri.
Mbowe: Mazungumzo yameshafanywa hivyo hawezi kuongea na amesema kuhusu picha za Lowassa kuwa kwenye kikao cha CHADEMA zimetengenezwa.
Lipumba
Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.
No comments:
Post a Comment