Thursday 9 July 2015

H baba Kurudi katika Ulimwengu wa Soka Kuichezea Toto Africa

Good news ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva, H Baba ambaye ametangaza rasmi sasa hivi kurudi kwenye soka na kujiunga na timu ya Toto African.

‘Kupitia kwenye kipindi cha AMPLIFAYA cha Clouds FM july 7, 2015 alifunguka na kusema’Ni kweli kwamba mimi nina vipaji vingi sasa ubora wa vipaji ni kuvionesha kwasababu nilishawahi kucheza soka na hii ni timu ya nyumbani timu nyingi zilishawahi kunihitaji sema muda mwingi sana nilikua kwenye kazi zangu za muziki kwa hiyo kwasasa hivi najipanga kwa mambo mengi wasishangae nikafanya vitu tofauti’– H Baba
‘Hapana siwezi kuacha muziki siwezi kuacha mpira siwezi kuacha filamu ni vitu vyote ambayo ninavyovipenda na siwezi kuja kuviacha mimi umri wangu bado mdogo unaniruhusu kuingia kwenye soka kwasasa hivi mimi niko Toto African watu wajiandae tu wafahamu kuwa niko Toto ila bado tupo katika harakati kwamba tutakapokaa sawa kuzungumza yakifikia sasa maafikiano ila Yanga na Sima wajiandae’ – H baba

No comments: