Wednesday, 22 July 2015

Kiongozi wa Al-Quaeda auawa

Muhsin al-Fadhli
Jeshi la Marekani linasema kuwa mmoja viongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, ameuwaua katika shambulio la angani lililotekelezwa na ndege za kijeshi za Marekani Nchini Syria.
Idara ya ulinzi ya Pentagon imesema kuwa Muhsin al-Fadhli, alikuwa kinara wa kundi la Khorasan, lililotumwa na al-Qaeda, kutoka Pakistan hadi nchini Syria.

Mmoja wa wajumbe wa bunge la congress amesema kuawawa kwa mtu huyo Al Fahdli mwenye ufahamu na gaidi hatari ambaye amekuwa akijaribu kuiangamiza Marekani na washirika wake ni faraja kubwa.
Al Fahdli anajulikana kama mtu muhimu katika Khorasan ambao ni mtandao muhumu kwa kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo lilikuwa likitumwa kutokea Pakistani na Syria kwa ajili ya kufanya mashambulizi ya kigaidi kwa nchi za magharibi.
Mfadhili huyo mkubwa wa kundi la kigaidi amekuwa akitafutwa na marekani kwa mara kadhaa ambapo Marekani ilitangaza kitita cha dola milioni saba kwa yoyote atakayefanikishwa kuauwa kwake.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon anasema Al Fahdli alikuwa miongoni mwa watu wachache wanaoaminiwa na kiongozi wa Al Qaeda ambaye pia aliwahi kupewa taarifa za kutokea kwa shambulio la kigaidi septemba 11 huko Marekani.
Taarifa za kifo chache zilisambazwa tangu mwaka jana lakini ni sasa imethibitishwa kuwa Al Fahdli ameuawa Julai 8 mwaka huu huko Syria.

No comments: