Ubalozi
wa Tanzania nchini Uganda umeikirimu timu ya taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) chakula cha jioni baada ya timu hiyo kutolewa na Uganda (The
Cranes) katika kinyang'anyiro cha kugombania nafasi ya kucheza fainali
cha CHAN mwakani nchini Rwnada.
Katika mechi hiyo ya marudiano
iliyochezwa katika uwanja wa Nakivubo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na
Tanzania kuanga michuano hiyo, baada ya kipigo cha magoli 3-0
ilichokipata kutoka kwa Uganda wiki mbili zilizopita mjini Zanzibar.
Stars ilialikwa chakula cha jioni na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania
iliyopo jijini Kampala.Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, wenyeji wakiwemo maofisa wa ubalozi , watanzania waishio nchini Uganda waliwapongeza wachezaji, viongozi kwa mchezo mzuri dhidi ya Uganda na kuwatakia kila la kheri katika safari ya jumatatu ya kurejea jijini Dar es salaam ikitokea Uganda kwa Shirika la ndege la Rwandair.
No comments:
Post a Comment