Tuesday, 7 July 2015

Rais wa Uganda ateuliwa kuwa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi

Rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni, ameteuliwa kuwa msuluhishi mpya katika mgogoro wa Burundi.Viongozi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki wamemteua Jumatatu wiki hii katika mkutano wao jijini Dar es Salaam,
 rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni, kuwa msuluhishi mpya wa mgogoro unaoendelea nchini Burundi.

Mgogoro huo ulizuka wakati rais Pierre Nkurunziza alitangaza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais.
Hata hivyo rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakushiriki mkutano huo wa marais. Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki wameitaka kwa mara nyingine tena serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi wa urais hadi Julai 30. Hata hivyo uchaguzi wa urais nchini Burundi umepangwa kufanyika tarehe 15 Juni mwaka huu.
" Pendekezo hilo la kuahirisha uchaguzi kwa kipindi chote hicho ni kutaka kumpa muda msuluhishi huyo mpya kuongoza mazungumzo ”, amesema katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera, baada tu ya mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Taarifa ambayo haijathibitishwa inaarifu kwamba huenda msuluhishi wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily amejiuzulu kwenye nafasi hiyo.
Haijafahamika iwapo serikali ya Burundi itakubali kuahirisha uchaguzi wa urais, kwani hata awali Umoja wa afrika uliiomba serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi wa wabunge na madiwani na ule wa urais, lakini uchaguzi wa wabunge namadiwani ulifanyika Juni 29, na uchaguzi wa urais unatazamiwa kufanyika Julai 15.

No comments: