Licha ya kuwepo kwa malalamiko tangu siku ya kwanza ya zoezi hili
kuanza hapa jijini lakini mamlaka husika zimeonekana kushindwa kuyatatua
kwa wakati hali inayopelekea msongamano kwa baadhi ya vituo
kutokupungua na watu kulazimika kuamka usiku wa manane kuwahi namba za
uandikishwaji siku moja kabla.
TanzaniaOne blog imetembelea vituo mbalimbali na kushuhudia wananchi wakiwa
wamejipumzisha vivulini na wengine wakichapa usingizi wakisubiri kuitwa
majina huku kina mama wenye watoto wakilalamikia kutokupewa kipaumbele.
Baadhi ya waandikishaji waliozungumza na Ukomboz Blog wamedai kuwa tatizo la
vidole vya baadhi ya wananchi kutokusoma kwenye mashine limekuwa
likijitokeza mara kwa mara na kulazimika kutumia muda mwingi kuhudumia
mtu mmoja hali inayozua kelele kwa watu waliopo kwenye foleni.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke akizungumzia zoezi hilo
amesema changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo mara kwa mara ni
watu kupiga simu vituoni hasa wanapoona wenzao hawafuati utaratibu na
kuongeza kuwa hakuna aliyeshikiliwa kutokana na vurugu zinazojitokeza
katika vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment