Ndege za majeshi ya muungano |
Ushirikiano unaoongozwa na Marekani, unasema kuwa umefanya mashambulio
makubwa ya ndege dhidi ya shina la wapiganaji wa Islamic State, katika
mji wa Raqqa, wa Syria.
Msemaji wa Marekani, alieleza kuwa ndege
zilishambulia mara 16, maeneo ya IS, kwenye moja kati ya operesheni
kubwa kabisa ya ndege kufanywa nchini Syria.Wapiganaji wa IS waudhibiti mji wa Raqqa |
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Syria, limesema kuwa shambulio la ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani, ilipiga shule mjini Raqqa, na kuuwa raia watano, pamoja na mtoto, na mpiganaji mmoja wa IS.
No comments:
Post a Comment