Maafisa
wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana
kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania.
Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam.Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.
Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Kwa mujibu na raia wanoishi karibu na kituo hicho,makabiliano ya risasi yalidumu kwa zaidi ya saa moja.
Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo akisema askari 4 na raia 3 wameaga dunia.
Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.
Aidha amesema kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.
Hakuna aliyekamatwa kufuatia shambulizi hilo japo maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.
Kulikuwa na matone ya damu nje ya kituo hicho cha polisi dalili kuwa waliojeruhiwa walikuwa wakijaribu kutafuta msaada.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo japo bwana Mangu anasema kuwa ni mapema mno kusema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi.
Hii si mara ya kwanza kwa kituo cha polisi kuvamiwa, mwaka uliopita kundi la watu waliokuwa wamejihami lilivamia kituo cha polisi na kukimbilia mwituni.
No comments:
Post a Comment