Tuesday 7 July 2015

Israel nembo ya ufuska na ufisadi

Israel nembo ya ufuska na ufisadiTaarifa mbalimbali zinaashiria kuwepo ufisadi mkubwa katika sehemu mbalimbali za utawala wa Kizayuni wa Israel, likiwemo jeshi na polisi ya utawala huo na jambo hilo kwa mara nyingine tena limezishangaza fikra za walio wengi kutokana na ukubwa wa ufisadi unaofanyika ndani ya utawala huo haramu. Ufisadi umekita sana mizizi ndani ya utawala wa Kizayuni kwa kadiri kwamba hivi sasa umeenea katika sekta zote za utawala huo na tatizo hili ambalo chanzo chake ni utambulisho ulio dhidi ya maadili wa utawala wa Kizayuni, limeathiri pia nyanja mbalimbali za utawala huo zikiwemo za kisiasa na kijamii.
Kuhusiana na suala hilo, naibu msemaji wa bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel amesema ufisadi na ufuska wa kingono umeeneza sana kati ya wanajeshi wa utawala huo. Bezalel Smotrich ametahadharisha kuhusu hatari ya kesi ya ufisadi wa kiakhlaki katika jeshi la utawala wa Israel na kueleza kuwa: Suala la kuwaajiri wanawake jeshini linapasa kusimamishwa.
Huko nyuma pia maafisa wa ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa jeshi la Israel walieleza wasiwasi wao kuhusu ongezeko kubwa la uhalifu hususan ufuska kati ya wanajeshi wa Israel na kusisitiza kuwa, tatizo hilo kubwa limeziweka taasisi muhimu za utawala huo katika ncha ya kusambaratika.
Kuongezeka vitendo vya ufisadi na ufuska katika jeshi la Israel kunazungumziwa sasa katika hali ambayo makumi ya maafisa wa kisiasa wa zamani na wa sasa wa utawala huo pia miaka kadhaa iliyopita walishatuhumiwa na vyombo vya sheria kwa makosa mbalimbali ya ufisadi wa fedha na kingono. Afisa mmoja wa kitengo cha kupambana na ufisadi cha polisi ya utawala wa Kizayuni wa Israel pia alijiuwa baada ya kutuhumiwa kwa kula rushwa. Afrim Bracha ambaye alikuwa miongoni mwa wapepelezi mashuhuri na Naibu Kamishna wa Polisi wa utawala wa Israel ambaye alikuwa akikabiliwa na tuhuma kadhaa za kula rushwa na ufisadi wa fedha, aliamua kujiuwa kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa mahakamani.
Kuongezeka sana vitendo vya uhalifu na kuenea ufuska ndani ya jeshi la utawala wa Kizayuni ni changamoto kubwa inayoutatiza utawala huo ghasibu. Tovuti ya habari ya Kizayuni ya Walla ilifichua katika ripoti yake mpya ikinukuu mahakama ya kijeshi ya Israel kuwa: Vitendo vya uhalifu vilivyofanywa mwaka jana wa 2014 vilikuwa vingi kwa kadiri kwamba katika muda huo ufisadi wa ngono na uuzaji haramu wa silaha uliongezeka kwa asilimia 63 na 75 kwa utaratibu ikilinganishwa na mwaka juzi wa 2013.
Kwa sasa hakuna siku inayopita bila ya kutangazwa habari kuhusu hali mbaya ya ufuska na ufisadi wa fedha, akhlaki, na otovu wa maadili ndani ya jamii ya Kizayuni ya Israel na kimsingi ufisadi uliopo ndani ya jamii ya Kizayuni ni miongoni mwa sifa kuu za utawala huo.

No comments: