Thursday 30 July 2015

Wafuasi 3 wa CCM wajeruhiwa katika ugomvi wa kisiasa wilayani Rorya.

Watu watatu wamelazwa katika hospitali teule ya Shirati wilayani Rorya baada ya kujeruhiwa vibaya katika ugomvi ambao unadaiwa kuhusishwa na kampeni za kisiasa za wagombea wa ubunge wa chama cha mapindizikatika jimbo la Rorya mkoani Mara.
Mmoja wa majeruhi wa tukio hilo, amesema walishambuliwa na chupa huku wakitishiwa kukatwa mapanga muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa kampeni za CCM katika eneo hilo. 

Hata hivyo mwenyekiti wa CCM wilayaya Rorya Bw Samwel Kiboye, amekiri kupata taarifa hizo kuhusu wafuasi wa mmoja ya wagombea kununuliwa silaha za jadi kwa ajili ya kuwashambulia vijana wa wagombea wengine na kusema mbali na tukio hilo kufikishwa katika vyombo vya dola pia chama hicho kitachukua hatua kali kwa wahusika huku mmoja wagombea Mh Lameck Airo akitishia kujitoa kugombea ubunge endapo vitendo hivyo havitadhibitiwa.

No comments: