Thursday, 29 September 2016

Raia wa Uganda Alfred Olango auawa na polisi Marekani

El CajonPolisi wamekiri kwamba Olango hakuwa na silaha
Polisi katika jimbo la California, Marekani wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mkimbizi wa Uganda ambaye wanasema alitoa kifaa chenye ncha kali mfukoni na kuwalekezea maafisa "kana kwamba alikuwa anawafyatulia risasi."
Baadaye, imebainika kwamba ilikuwa ni sigara ya kisasa ifahamikayo kama 'e-cigarette'.
Waandamanaji kadha wamejitokeza katika barabara za El Cajon, viungani mwa mji wa San Diego, kulalamikia kuuawa kwa Alfred Okwera Olanfo, aliyekuwa na umri wa miaka 38.
Bw Olango aliuawa Jumanne baada ya polisi kujibu wito kutoka kwa dadake Olanfo ambaye aliitisha msaada.

Arsenal yainyuka 2-0 Basel,

ArsenalTheo Walcott
Michuano ya klab bingwa barani ulaya inaendelea katika hatua ya makundi ambapo Usiku wa kuamkia leo michezo michezo nane ilipigwa katika viwanja tofauti.
Arsenal ikiwa nyumbani ilibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Basel ya nchini uswizi, magoli yote yaliwekwa kimyani na Theo Walcott.
PSG ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.
Borussia Moenchengladbach nayo ikiwa nyumabi imekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Barcelona. Na mchezo wa kushangaza wa funga nikufunge ulikuwa kati ya Celtic na Manchester City, ambazo zilienda sare ya 3-3.
Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven