Shilole amekumbwa na dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole kujihusisha na shughuli za sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwanamuziki
huyo anayejulikana pia kama Shishi Baby amekumbwa na dhahama hiyo baada
ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha akicheza jukwaani akiwa katika
mavazi yanayokinzana na maadili ya Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.
Katibu
Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amezungumza na Mwananchi Digital
kwa njia ya simu leo na kusema hatua hiyo imechukuliwa baada ya awali
kumpa onyo kwa matukio ya kupanda jukwaani kufanya sanaa akiwa katika
mavazi yasiyozingatia maadili ya Kitanzania.
“Awali
tulimuonya kwa vitendo hivi, akakiri kosa na kuahidi kwa maandishi kuwa
hatarudia kufanya hivyo” alisema na kuongeza: “Hata hivyo, wadau wa
muziki watakumbuka alichokifanya nchini Ubelgiji. Lilikuwa tukio la aibu
kwake kama msanii, aibu kama mwanamke na aibu kama Mtanzania” alisema.
Amewataka
wasanii kujitathimini kabla ya kupanda jukwaani na kuonya kuwa Basata
itaendelea kuchukua hatua kama hizo dhidi ya msanii yeyote
atakayebainika kuvunja/kukiuka maadili ya nchi. Shilole amekiri kupokea
barua kutoka Basata akisema, hivi sasa yuko kwenye majadiliano na
mwanasheria wake na kusema anakusudia kukata rufaa kupinga kufungiwa
huko. “Mashabiki wangu watulie kwani hii ni changamoto, tunaifanyia kazi
kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni” alisema.
No comments:
Post a Comment