Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Lubambangwe nje kidogo ya
mji wa Chato ambapo basi la Sabuni Express lenye namba za usajili T275
AZG likitokea mji mdogo wa mugaza kuelekea jijini Mwanza limepata ajali
mbaya katika barabara ya buzirayombo kyemirwa baada ya kugongana na
magari mawili ya mizigo aina ya Scania na kusababisha kifo cha mtu mmoja
na wenguine 30 kujeruhiwa vibaya ambapo baadhi ya majeruhi wamevunjika
miguu na mikono huku mama mmoja mwenye watoto watatu aliyenusulika kifo
katika ajali hiyo akikatiza safari na kurudi nyumbani kwake.
Akizungumza na ITV mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Chato
Dr.Pius Buchukundi amesema kuwa amepokea majeruhi 31 kati yao mmoja
akafariki dunia wakati akitibiwa huku majeruhi wawili wakizidiwa na
kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza
kwa matibabu zaidi na kwamba majeruhi 20 wametibiwa na kuruhusiwa ambapo
wagonjwa tisa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya
Chato na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment