Wednesday 12 August 2015

Vifungu vyote vya sheria ya mtandao vilivyolalamikiwa na wadau vimerekebishwa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dk Ally Simba amesema vifungu vyote vilivyolalamikiwa na wadau kuhusu sheria ya makosa ya mtandao vimefanyiwa marekebisho huku akiwataka wananchi hasa watumiaji wa mitandao kujiandaa kuipokea sheria hiyo.
Rai hiyo imekuja zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba mosi mwaka huu ambapo amesema kuanza kwa sheria hiyo kutasaidia mambo mengi sana ikiwemo kulinda mifumo ya msingi ya tehama na kutolea mfano wa mitandao ya simu za mkononi.
 
Kwa upande wake mtendaji mkuu wakala wa serikali mtandaoni Bw Jabri Bakari kwa sasa serikali inajitihadi kushirikiana na wadau wa sekta binafsi hasa wataalam wanaoshughulikia mifumo ya komputa kuhakikisha wanakutana mara kwa mara kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu wa suala la usalama wa mitandao.

No comments: