Klabu ya Chelsea inatarajiwa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu
aliyoonyeshwa mlinda mlango Thibaut Courtois katika mchezo uliopigwa
jumamosi dhidi ya Swansea ambao uliisha kwa droo ya magoli mawili katika
uwanj wao wa nyumbani Stamford Bridge.
Mchezaji huyo wa
kimataifa wa Ubelgiji huyo mwenye umri wa miaka 23 alitolewa nje dakika
ya 52 baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji Bafetimbi Gomis wa Swansea
ambaye alikua anakwenda kushinda ambapo Swansea walipata penalti
kutokana na faulo hiyo.Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kuongelea uamuzi huo baada ya kipute cha mwisho. Rufaa ya Chelsea itasikilizwa na chama cha soka nchini Uingereza FA siku ya jumanne.
Iwapo rufaa hiyo itakataliwa, Courtois ambaye anatarajiwa kufungiwa mchezo mmoja atakosekana katika safari ya kuwakabili washindi wa pili kwenye msimu uliopita Manchester City jumapili ijayo.
ikumbukwe kwamba,Asmir Begovic aliyesajiliwa kutoka klabu ya Stoke aliichezea Chelsea kwa mara ya kwanza dhidi ya Swansea baada ya kutolewa nje Courtois.
No comments:
Post a Comment