Polisi waliwazuia wanachama wa Chadema na Ukawa ambao
waliandamana na msafara wa Mh. Lowasa kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mkoan
Kilamanjaro KIA, walipofika maeneo ya jimbo la Arumeru mashariki mji mdogo wa
USA River karibu na Mto nduruma walikuta jeshi la polisi wakiwa wameweka
vizuizi na kuanza kurusha mabomu ya machozi kuwatawanyisha wanachama wa Ukawa
walioandamana na Lowasa.
Lema aliendelea kusema “serikali na jeshi la polisi wanajaribu
kuwaogopesha wananchi ili ccm waweze kuiba kura uchaguzi ujao “ Pia atoa salamu
kwa IGP wa Arusha “ Kama amewafundisha
wanajeshi wake kuuwa basi yeye kajifunza kutembea akiwa maiti “
Lema akizungumzia swala la Jeshi la Polisi la Mkoa wa
Kilimanjaro kumzuia Lowasa kwenda kumzika aliyekuwa mwanachama wa chama cha
Mapinduzi Mzee Kisumo Alisema
haoni sababu ya maana ya lowasa kuzuiliwa kwenda msibani kwani haijawahi
tokea duniani mtu akazuiliwa kwenda msibani
bali anahisi ni woga wa Rais Jakaya Kikwete kuwa atafunikwa na Lowasa
katika msiba huo.
Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia nae awaonya jeshi la
polisi kwa kuwaasa mkuu wa jeshi la Tanzania Mangu kuwa kama wataendelea
kuwaonea wananchi kwa kuwapiga mabomu ovyo ovyo basi wasubirie mahakama ya ICC
kuwatia mbaroni
Licha ya kuwaasa wakuu wa jeshi la polisi amemwaga sifa kwa
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa kusimamia Mkutano wao kwa makini na bila
Uonevu wa aina yoyote
No comments:
Post a Comment