Siku
moja baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura za maoni ndani ya
CCM na kushindwa, mbunge wa jimbo la Segerea Mh Makongoro Mahanga
ametanagza kukihama chama cha CCM na kujiunga na chama cha Chadema baada
ya kutokutendewa haki katika mchakato huo.
Ukandamizaji wa democrasia ndani ya CCM, ni moja ya sababu
zilizomfanya naibu huyo wazir wa kazi na ajira kuamua kukikacha chama
chake cha CCM, lakini wadadisi wa siasa za Tanzania wanabashiri huenda
hii ikawa miongoni mwa sababu kuu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini
Dar es Salaam Dkt Militon Makongoro Mahanga amesema kushindwa kwake
kwenye kura za maoni kunatokana na hujuma na upendeleo uliofanywa na
uongozi wa CCM wilaya ya Ilala kwa moja ya mgombea wa nafasi hiyo.
Anasema baada ya kujiridhisha nambinu zote chafu zilizotumiwa na
baadhi ya wagombea dhidi yake, na pia kujiridhisha bila shaka na namna
viongozi wa CCM wanavyompiga vita tangu mwaka 2000 sasa anasema
inatosha.
Katika mkutano huo pia amekiri kuwa na mahusiano ya akribu na
waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowasa nakwamba kama viongozi wa Chadema
watamkubali anaamini atakuwa sehemu salama zaidi katika harakati zake za
kisiasa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment