Monday 12 May 2014

Abiria apindua gari


WATU wasiozidi 50 wamenusurika kifo baada ya basi dogo kupinduka katika eneo la Sinai nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma kutokana na uzembe wa abiria .Ajali hiyo ilisababisha na mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni askari wa jeshi la kujenga Taifa JKT Mlale Songea ambaye alikuwa ni mmoja wa abiria kuamua kuendesha basi hilo baada ya dereva wa basi kuteremka na kumsaidia  dereva mwenzake ambaye basi lake lilikuwa limeharibika.Dereva wa basi lililopata ajali Bernad Bernad maarufu kwa jina la Kichefuchefu alisema yeye baada ya kutelemka kwenda kumsaidia dereva mwenzake alishangaa kuona gari lake linarudi nyuma likiendesha na mmoja wa abiria kisha kupinduka baada ya  abiria huyo anayedaiwa kuwa ni mwanajeshi kushindwa kulimudu kuendesha

No comments: