Galatasaray waibuka mabingwa wa kombe la Ziraat nchini Uturuki.
Galatasaray walinyakuwa ubingwa huo baada kuilaza timu ya soka ya Eskisehirspor kwa bao 1-0.
Kwa matokeo hayo, timu ya Galatasarary imefanikiwa kukomesha ukame wa kutochukuwa kombe hili kwa miaka 9.
Waziri wa vijana na michezo bwana Akif Cagatay ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Konya ambapo wachezaji hao wa sare za njano na nyekundu walipokea kombe kutoka mikononi mwake.
Kwa sasa, Galatasaray wanajivunia kuchukuwa kombe hili kwa mara ya 15.
Rais Abdullah Gul amemtumia rais wa klabu bingwa bwana Unal Aysal ujumbe wa pongezi kwa njia ya telegraf ili kuwapongeza wachezaji, kamati ya ufundi na wahusika wa uongozi wote kwa ujumla.
Vile vile waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan alimtumia bwana Unal Aysal ujumbe baada ya ushindi wa klabu.
No comments:
Post a Comment