Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis |
Kamati ya Umoja wa Mataifa
dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia
ipasavyo suala la unyanyasaji wa ngono ndani ya kanisa hilo.
Vatican inapuuza haki za watoto
Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatcan umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayaendani na vitendo .
Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.
Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatican ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.
No comments:
Post a Comment