wachezaji wa Mbeya city |
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alitangaza
uteuzi huo kwa waandishi wa habari jijini Mbeya mara baada ya kufanya
kazi ya kukagua Uwanja wa Sokoine kama unafaa kuchezewa mechi za
kimataifa, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, mashindano hayo
mapya hushirikisha timu zilizoshika nafasi ya pili katika ligi za nchi
wanachama, ambapo kwa Tanzania, Yanga ndiyo ilitakiwa kushiriki michuano
hiyo, lakini walisema hawapo tayari kushiriki.
Alisema kuwa hata walipoiteua timu ya Azam ambayo
ndiyo mabingwa wa Ligi ya Tanzania Bara waligoma kushiriki wakidai kuwa
wachezaji wao wapo likizo.
Alisema kuwa Cecafa kwa kushirikiana na TFF waliona ni vyema kuiteua Mbeya City ambayo imeshika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment