Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei
alisema dereva huyo aliyekuwa alikitoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC), alikutwa na mauti hayo akiwa ndani ya gari aina ya Leyland Daf
alilokuwa akiendesha kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda Matei alisema kabla ya dereva huyo
mwenyeji wa Mkoa wa Iringa kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa
akilalamika kuwa anajisikia vibaya walipokuwa njiani.
Akizungumzia tukio hilo utingo wa lori hilo, Said
Hemed (22) alisema: “Tulianza safari vyema, lakini tulipokaribia
Chalinze, akaanza kulalamika kuwa hajisikii vizuri. Tuliendelea na
safari, huku nampa moyo lakini alirudia maneno hayo tulipofika Mlandizi,
lakini alikuwa akinieleza itambidi kwenda kupima pindi akifika tu Dar
es Salaam.
“Tukaendelea na safari na jamaa alikua safi tu
akiendesha, lakini tulipokuwa kati ya Mlandizi na Kibaha alirudia kusema
mwili wake kama haupo vizuri vile na tulipokuwa katikati ya safari
kabla ya kufika Misugusugu aliniambia... ‘Dogo hali siyo nzuri ninaumwa
aisee’.
“Nikamuuliza sasa kuendesha utaweza kweli?
Akaniambia Mungu ni mwema, nitajitahidi tufike Dar es Salaam ili
nikafanye vipimo kabisa maana hali siyo nzuri. Tukaja hadi hapa check
point (kituo cha ukaguzi) sasa akawa ananieleza huku kalalia usukani.
Mimi nikateremka kuangalia kinachoendelea, kwani ilikuwa foleni ndefu
kiasi. Muda mfupi nikarudi kwenye gari, kufika nikamkuta ‘bro’
amefariki, yaani ni kama kaniambia hebu nipishe naondoka. Sikuamini
lakini ndivyo ilivyotokea.”
Kamanda Matei alisema kuwa mwili wa marehemu
ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya kuhifadhiwa
pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Ofisa Habari wa Hospitali ya Tumbi, Gerald Chami alisema vipimo vilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Hemed alisema baadaye kuwa baada ya tukio hilo
alifanya utaratibu wa kuliingiza lori hilo katika yadi ya magari iliyopo
eneo hilo na baadaye kufanya mawasiliano na tajiri yake kwa ajili ya
utaratibu wa kuuhifadhi mwili pamoja na gari.
No comments:
Post a Comment