Mwanaharakati anaeunga mkono urusi, katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine.
Watu 40, wakiwemo wapiganaji 38 na raia wawili wameuawa
jumanne hii katika mapigano kati ya jeshi na waasi wa Ukraine yalioanza
jumatatu wiki hii katika jitihada za kujaribu kilia upande kudhibiti
uanja wa ndege wa Donetsk katika eneo la mashariki, mkuu wa manispa ya
jiji la Donetsk amethibitisha.
|
Helikopta
ya jeshi la Ukraine aina ya Mi-24 ikitumiwa katika mapigano ili
kujaribu kuondoa uwanja wa ndege wa Donetsk mikononi mwa waasi
waliyouteka hivi karibuni, Mei 26 mwaka 2014.
|
|
Viongozi wa Kiev wamethibitisha kwamba wameurejesha kwenye himaya ya utawala uwanja huo.
Wakati huo huo Urusi imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine.
“ Jukumu la kwanza na mshikamano wa viongozi wa
|
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergueï Lavrov akitolea wito pande zote kusitisha mapigano nchini Ukraine.
|
|
Kiev,
kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais, ni kusitisha kutumia jeshi kwa
kukandamiza raia pamoja na pande zote mbili kusitisha machafuko, amesema
waziri wa mambo ya kigeni wa urusi”, Sergueï Lavrov.
Hato yakijiri waziri mkuu wa Ukraine Arseni Iatseniouk, ametupilia
mbali uwezekano wa kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi ili
kujaribu kukomesha machafuko ambayo yanaendelea kuathiri taifa la
Ukraine, bila hata hivo kuweko kwa wasuluhishi kutoka mataifa ya
magharibi.
|
Waziri mkuu wa Ukraine Arseni Iatseniouk amekataa katakata mazungumzo na Urusi.
|
|
“Kwa sasa mazungu kati ya Urusi na Ukraine hayawezekani iwapo
Marekani na Umoja wa Ulaya havitaashirikishwa” amesema Iatseniouk katika
kikao cha baraza la mawaziri, huku akibaini kwamba wanahofia
kudanganywa na Urusi iwapo wataketi pamoja kwenye meza ya mazungumzo.
Jumatatu wiki hii rais mpya wa Ukraine Poroncheko amethibitisha
kwamba amekua na matumaini ya kukutanakwa mazungumzo na rais wa Urusi
Vladimir Putin, na mkutano huo ungeliandaliwa katikamwezi ujao.
No comments:
Post a Comment