Msemaji
wa kikosi cha jeshi la wanamaji cha Libya aliwaambia waandishi wa
habari kupitia taarifa kuwa miili 32 ilipatikana baada ya jeshi la
wanamaji kuvunja na kuingia katika chombo kilichozama.
Msemaji wa kikosi cha jeshi la wanamaji cha Libya Colonel Eyup Kasim aliwaambia waandishi wa habari kupitia taarifa kuwa miili 32 ilipatikana baada ya jeshi la wanamaji kuvunja na kuingia katika chombo kilichozama.
Siku ya alhamisi chombo hicho kilichokuwa kinasafirisha wahamiaji haramu 130 kilizama baharini karibu na ufuo wa Libya na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine 74 kutoweka. Juhudi za kuwatafuta waathiriwa hao bado zinaendelea.
Watu 52 waliokolewa kutoka kwenye mashua iliyozama.
No comments:
Post a Comment