Operesheni
dhidi ya Taliban katika mkoa wa Ghazni wa Afghanistan ulisababisha
kuuawa kwa wanamgambo 63 wa kundi hilo katika wiki ya mwisho.
Taarifa iliyoandikwa kutoka Wizara ya ndani ya Afghanistan ilisema vikosi vya usalama viliweza kuwaua wanamgambo 63 wa Kitaliban katika Oparesheni iliyofanyika katika mkoa wa Ghazni.
Iliripotiwa kuwa wanamgambo 21 kati ya waliouawa ni raia wa kigeni waliokuwa wamejiunga na kundi hilo.
No comments:
Post a Comment