BELO HORIZONTE, BRAZIL
DUNIA imeshavua nguo na sasa kilichobaki ni
ufirauni. Atakayekwenda kushuhudia fainali za Kombe la Dunia nchini
Brazil atakumbana na mabadiliko makubwa ya maisha ya kidunia nchini
humo.
Wanawake katika mji wa Belo Horizonte uliopo maili
270 kutoka katika Mji Mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro wamefurahishwa na
kaulimbiu ya mtindo huo wa malipo ambao umepachikwa jina la “Furahia
sasa, lipia baadaye”.
Cida Vieira, malaya wa kundi la makahaba
linalofahamika kama Aprosmig, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Malaya
katika jimbo la Minas Gerais alidai kwamba kwa sasa hakutakuwa na
kukabana koo dhidi ya wateja ambao hawana pesa mifukoni lakini wanazo
katika akaunti zao.
“Wateja wanaotaka kuendelea na starehe zao lakini
hawana pesa taslimu mifukoni, wanaweza kuendelea kula raha bila ya
kuingiliwa,” alisema Cida ambaye ni malaya maarufu wa maeneo hayo.
Kwa mujibu wa kundi hilo, wamedai kwamba malipo ya
kupitia kadi yanaleta usalama kwa mteja na vilevile taarifa za matumizi
ya mteja hazitaeleza sababu hasa za matumizi yake katika pesa
zilizotoka kwenda kwa malaya.
Wajifunza Kiingereza
Wakati michuano hiyo ikiwa imebakisha siku chache
kuanza huku ligi mbalimbali barani Ulaya zikiwa zinafikia ukingoni,
baadhi ya malaya wameanza kujifunza lugha ya Kiingereza kwa ajili ya
kunasa wateja ambao hawafahamu lugha ya Kireno.
Tangu mwaka jana, malaya hao wa Brazil wamekuwa
wakijiunga katika madarasa mbalimbali ya Kiingereza nchini humo kwa
ajili ya kujifunza lugha hiyo ambayo itawarahisishia majadiliano na
wateja wao wanaotumia lugha ya Kiingereza.
“Hii ni muhimu kwa heshima ya ya kazi hii.
Wanawake wanapaswa kujadiliana bei na mteja na kujitetea wenyewe,”
aliongeza Cida. Umalaya umehalalishwa nchini Brazil na wanawake nchini
humo wanatazamia mapato makubwa wakati wa Kombe la Dunia.
Kundi hilo la malaya pia linatazamia kujifunza
lugha mbalimbali wakiwa darasani kama vile Kihispaniola, Kiitaliano,
Kifaransa na hata Kireno kwa malaya ambao wamezamia nchini humo, lakini
hawaifahamu lugha hiyo inayotumiwa zaidi na Wabrazili.
Mpaka Juni mwaka jana, Vieira anadai malaya 20 walikuwa
wamejiunga katika madarasa hayo, lakini alikuwa anatazamia kuwa malaya
wengine 300 wangejiunga katika kundi lao lenye malaya 4,000.
Waingereza waonywa na polisi wao
Polisi nchini Uingereza imewaonya mashabiki wa
soka nchini humo kuwa Polisi wa Brazil wanawasubiri kwa hamu mashabiki
ambao watafanya ngono na watoto wadogo nchini humo kwa ajili ya
kuwapeleka jela.
Mashabiki hao wa England wameambiwa kuwa watazamie
vifungo vya gerezani nchini Brazil au Uingereza kwa kufanya ngono na
watoto wadogo ambao wamekuwa tatizo kubwa katika nchi hiyo ya Amerika
Kusini.
Ripoti kutoka Brazil zinadai kuwa watoto wenye
umri mdogo hata wa kufikia miaka 11 huwa wanavaa nguo ambazo zinawafanya
waonekane wakubwa kwa ajili ya kufanya biashara ya ngono. Ni marufuku
nchini humo kulipia huduma ya ngono kwa msichana mwenye umri chini ya
miaka 17.
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, pamoja na
ile ya Olimpiki miaka miwili ijayo inatazamiwa kufichua kwa kiasi
kikubwa tatizo hili na polisi pamoja na vyombo vya dola nchini humo
vimejipanga kuchukua hatua madhubuti.
Brazil inashika nafasi ya pili nyuma ya Thailand kwa biashara ya ngono kwa watoto.
“Watoto wa Brazil wanaweza kuathirika kwa kiasi
kikubwa na biashara ya ngono na wanaweza kujibadilisha hili waonekane
wakubwa kuliko umri wao halisi,” alisema Johnny Gwynne, ambaye ni mkubwa
kitengo cha kuzuia masuala hayo.
Uhalifu wa ngono unatajwa kuwa wa pili kwa ukubwa
nchini humo huku waathirika wakubwa wakiwa watoto wenye umri kati ya
miaka 10 hadi 14. Zaidi ya wageni 600,000 wanatazamiwa kuhudhuria
fainali za Kombe la Dunia nchini humo ambalo linatazamiwa kuanza Juni
12.
No comments:
Post a Comment