Waziri Mkuu majaliwa akiwafariji wazazi walioko katika wodi ya wazazi katika hosipital ya Mout Meru |
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana katika
hali ya kushangaza alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya mkoa Mout
Meru iliyoko mkoani Arusha. Ikumbukwe kuwa waziri mkuu yuko Arusha kwa ziara za
kikazi.
Katika ziara hiyo ilitokana na malalamishi kutoka kwa
wananchi juzi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
kwamba hosipitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wanaozliwa katika
hospitali hyo.
Hata hivyo jana kwatika ziara hiyo waziri mkuu alishuhudia
wodi ya wajawazito kitanda kimoja kikilaza watu watatu , na kuagiza hospitali
za pembezoni kuboreshwa ili kupunguza msongamano wa wangonjwa mout meru.
Majaliwa akielekea katika Wodi ya wazazi |
Akizungumzia sakata la wizi wa watoto katika hospital hiyo
alivitaka vyombo husika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo hii inatokana
wiki kama mbili zilizopita mzazi walda Musa kutuhumu hospital hiyo kwa kumwibia
mwanae baada ya kujifungua “ Nilikuja hapa hospitali tarehe 4/10 na
kutoka 7/10 nilijifungua kwa njia ya upasuaji ndipo walipomchukua mwanangu kwa
madai wanampeleka katika chumba cha joto, siku ya kwanza akaja Mume wangu na
kwenda kumwona mwanangu , siku ya pili pia alienda kumwona na kumkuta mwanetu
ni mzima wa afya , Lakin siku ya tatu wakati tunatoka tulipotoka mimi na Mume
wangu tuienda kumchukua mtoto na kuambiwa mtoto alifariki na hatukupata hata
fulsa ya kuona hata mwili wake”
Dk. Jackline Urio Mganga mkuu mfawidhi wa Hospitali hiyo
alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alisema kuwa mtoto huyo baada ya kuzaliwa
alipoteza maisha na baadae mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment