Monday 1 December 2014

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana.

Yacine Brahimi ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa afrika wa BBC mwaka huu

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana. tuzo za BBc mchezaji bora wa mwaka hutolewa na shirika la utangazaji la uingereza BBC.Baada ya maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Yacine Brahimi
Aliingiza bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la dunia.
Hio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi wa soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.

No comments: