Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na
wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano katika mji wa Mombasa pwani ya
Kenya. Polisi walipambana na vijana walioingia katika Msikiti wa Swafaa
eneo la Kisauni na mpaka sasa zaidi ya vijana 400 wanashikiliwa tangu
kuanza kwa msako huo, mapema wiki hii.
Msikiti huo ulifungwa jana baada ya polisi kuuvamia
Jumatano, ambamo walipata magruneti, mabomu ya petroli na silaha
nyingine. Hali ya wasi wasi bado imetanda katika mji huo wa pwani.
Serikali imekwishafunga misikiti minne ambayo wanasema ina uhusiano wa
watu wenye misimamo mikali ya imani ya kidini. Pamoja na kukamata silaha mbalimbali, polisi pia
walikamata bendera nyeusi, alama ya kuunga mkono kundi la kigaidi la
Al-Shabab la nchini Somalia
Awali polisi mjini Mombasa
pwani ya Kenya walisema wamepata silaha nyingine zaidi yakiwemo mabomu
katika msikiti wa tatu ambao ulifanyiwa upekuzi
Msako huo katika
msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa
Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha ndani ya msikiti ambao
wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihami kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine.
Waziri
wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa
katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za
kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa
kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Viongozi wa kiisilamu
wamelaani misako hiyo katika Misikiti wakisema kuwa itachochea zaidi
vijana kuendeleza itikadi kali za kidini.
No comments:
Post a Comment