Friday 21 November 2014

Akimbia kilometa nane kwa kuwakwepa polisi

Mkimbiaji mkenua amekimbia kwa umbali wa kilomita nane akikwepa Polisi katika kaunti ya Bergan, New Jersey nchini Marekani.
Eric Kipkemei Chirchir ,31, alikuwa anatafutwa na polisi wa New Jersey baada ya kupata ripoti kuwa alimshika katika hali ya kudhalilisha msichana wa miaka 15.
Chirchir aliingia kwenye chumba cha wanawake katika kituo cha kufundishia mchezo wa golf
Msichana huyo aliweza kukimbia na kwenda kutoa taarifa kuhusu tukio hilo Polisi.
Polisi walipomfuata Chirchir katika kituo hicho,aliwakimbia umbali wa kilometa nane kuelekea kwake na kuacha baiskeli yake na begi.
Polisi walimkamata Chirchir baada ya kumkuta alipokuwa amejeificha, kwenye kabati la nguo la mtoto wake mwenye umri wa miaka sita.
Chirchir ambaye siku ya alhamisi anatimiza miaka 31 akiwa kizuizini,ameshtakiwa kwa kosa la udhalilishaji kijinsia, kugoma kufuata amri ya polisi na kuwakwepa polisi.
Kijana huyo anashilikiliwa katika jela ya kaunti ya Bergen.
Chirchir aliweka rekodi ya kukimbia kwa muda wa 7:50:06 kwa umbali wa mita 3000 mjini Torino, Italia mwezi June mwaka 2007.
Katika mbio za nusu marathon aliweka rekodi ya kukimbia kwa saa 1:02:13 mwezi desemba mwaka 2011 mjini Zhuhai, China.

No comments: