
Safari ya Manchester City kutwaa
ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya imeingia mikosi zaidi baada
usiku wa kuamkia leo kukubali kugaragazwa nyumbani Etihad na Warusi wa
CSKA Moscow na kuufanya kuwa usiku mbaya jijini Manchester.
Licha
ya kuruhusu mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyotiwa wavuni na
Seydou Doumbia pia viungo wake muhimu Yaya Toure na Fernandinho
walitolewa nje kwa kadi nyekundu na hivyo wataikosa mechi ngumu ijayo
dhidi ya Bayern Munich. Yaya Toure alisawazisha bao la kwanza la
Doumbia lakini haikusaidia kitu kwani mchezo wa chini ya kiwango
unaoikabili timu hiyo hivi karibuni umeigharimu katika kundi lake kiasi
cha kucheza mechi nne na kupata pointi mbili tu. City haijashinda hata
mechi moja na sasa wanapaswa kuzifunga Munich na Roma katika michezo
iliyosalia ili kupata njia ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.
Yaya
Toure amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa timu yake kwa kupewa kadi
nyekundu kwa mara ya kwanza akiichezea Man City. Mechi zingine za ligi
hiyo zilizopigwa jana usiku ni pamoja na ile ya Bayern Munich
iliyoifumua AS Roma 2-0 mjini Munich, Ajax Amsterdam ikiwa nyumbani
imesagwa 2-0 na Barcelona, huku NK Mariobor wakiibana mbavu Chelsea kwa
kufangana 1-1.
Shaktar Donetsk imeivurumisha BATE Borisov mabao
5-0 ilhali Paris Saint Germain imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0
mbele ya Apoel Nicosia. Mechi zinazofuata zitachezwa Novemba 25.
No comments:
Post a Comment