kaseja |
Niyonzima |
Niyonzima, kwa upande wake amekuwa akidai kutofurahia maisha anayoishi ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Kiungo huyo raia wa Rwanda ambaye mkataba wake
unafikia ukingoni, amesema kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba mwingine
wa kuitumikia klabu hiyo.
Tayari, kiungo huyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo
na klabu nyingine anayotaka kwenda kuichezea kutokana na mkataba wake
kubakiza miezi sita.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili, ameeleza
kushangazwa na kitendo cha kocha Marcio Maximo kumtoa kipindi cha pili
bila kuambiwa sababu ili ajirekebishe kwenye mechi nne mfululizo za Ligi
Kuu dhidi ya Stand United, Kagera, Simba, na Mgambo.
“Mimi ni mchezaji, ninaitumikia timu yangu ya
taifa (Amavubi), pia ni tegemeo katika timu hiyo, ninacheza dakika 90,
sasa iweje hapa Yanga natolewa kipindi cha pili?” Alihoji.
“Kitu kingine kinachonichosha Yanga ni uzushi, ule
ninaosambaziwa na baadhi ya wanachama (makomandoo) kuwa Kaseja
ananishawishi nisaini Simba, kwa kuwa tunalala chumba kimoja tunapokuwa
kambini,” alisema Niyonzima.
Mbali na Niyonzima, pia klabu hiyo huenda ikamkosa kipa Kaseja ambaye hajadaka mechi kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.
Inadaiwa kuwa kipa huyo yupo mbioni kurejea timu
yake ya zamani, Simba ikiwa ni pamoja na Mbuyu Twite ambaye naye amegoma
kusaini mkataba hadi pale uongozi utakampomtimizia masharti yake.
Twite, amebakiza miezi sita kaitka mkataba wake wa kuichezea Yanga.
No comments:
Post a Comment