Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .
Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William.Bi Abbott alipokea mafunzo ya upigaji mbizi katika kituo hicho kilicho katika ufuo wa bahari ya Loch Linnhe mnamo mwaka 2007 na kuwaomba wafanyakazi wa kituo hicho wamruhusu afanye harusi yake chini ya maji hayo.
Bwawa hilo, hutumiwa kutoa mafunzo kwa wapiga mbizi pamoja na kufanyia majaribio vifaa vipya. Picha hizi zimetolewa na kituo hicho.
Maharusi hao waliungana na marafiki wao Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien chini ya maji hayo.
Wote wanne walivalia vifaa vya kupigia mbizi pamoja na mavazi yao ya harusi.
Bi Abbott anafanya kazi katika kiwanda cha mafuta na gesi.
No comments:
Post a Comment