Maisha ni magumu kwa wakimbizi nchini Syria
Uingereza imesema kuwa itatoa hifadhi ya muda kwa mamia kadhaa ya wakimbizi wa Syria ambao wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya maisha.
Naibu waziri mkuu, Nick Clegg, amesema kuwa serikali ya muungano itatoa fursa ya kwanza kwa wanawake wanaokabiliwa na hatari ya kubakwa, wale waliobakwa tayari, wazee na watu wanaoishi na ulemavu.
Shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR, ambalo limetowa wito kwa mataifa ya magharibi kutoa hifadhi kwa wakimbizi alfu thelathini kutoka Syria, limechangamkia tangazo hilo la Uingereza.
Mwakilishi wa shirika hilo nchini Uingereza amesema ni jambo la kutia moyo na hatua muhimu ambayo itasaidia kutoa suluhu zinazohitajika kwa wakimbiizi ambao wameathirika na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Hadi kufikia sasa serikali ya Uingereza imekataa kuwapokea wakimbizi ikisisitiza badala yake, kwamba inatoa msaada wa karibu dola bilioni moja.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International, limekosoa vikali viongozi wa ulaya ambao walitoa ahadi ya kuwapokea wakimbizi alfu kumi na nne pekee, wakati mataifa jirani na Syria yanahifadhi karibu wakimbizi milioni mbili.
No comments:
Post a Comment