Sunday 26 January 2014

wenger ,Akili za Mourhno si nzuri


KOCHA, Arsene Wenger wa Arsenal hajapata jibu na bado anajiuliza kama akili ya Jose Mourinho inafanya kazi sawasawa kutokana na uamuzi wake wa kuwauzia Manchester United mchezaji Juan Mata.

Wenger hapati jibu juu ya uamuzi wa Mourinho kukubali kumpeleka Mata kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England.

Staa huyo Mhispaniola amekamilisha vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga Man United baada ya kukosa nafasi ya kucheza kwenye klabu ya Chelsea licha ya kuwahi kuwa mchezaji bora wa kikosi hicho kwa misimu miwili mfululizo kabla ya kurejea kwa Mourinho klabuni hapo.

Man United kwa sasa inajaribu kuboresha kikosi chao baada ya kuanza msimu vibaya wakiwa nafasi ya saba kwenye msimamo, pointi sita pungufu kuwamo kwenye nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Wenger alisema: “Nimeshangazwa sana Mata ameruhusiwa aondoke. Chelsea imewanufaisha moja kwa moja wapinzani. Hivi Chelsea haitacheza tena na Man United. Wangemuuza Mata basi wiki mbili zilizopita.” Mfaransa huyo Jumatano iliyopita alikuwa Hispania kuzitazama Barcelona na Levante zikimenyana kwenye Kombe la Mfalme ikiwa ni safari yake ya kusaka straika mpya.

No comments: