Monday 27 January 2014

Chelsea ya zamisha meli ya Stock city

Chelsea imeifunga Stoke City katika mechi ya Kombe la FA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jana.
Alikuwa ni mshambuliaji Mbrazil, Oscar ambaye aliweza kuitoa kifua mbele timu yake hiyo wakati alipoukwamisha mpira wavuni katika dakika ya 27.
Hadi mapumziko, Chelsea walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Chelsea ilicheza mechi hiyo siku moja baada ya kiungo wao mahiri, Juan Mata kuhamia Manchester United.
Baadhi ya washabiki wa timu hiyo walikumbuka namna ambavyo mchezaji huyo aliposhirikiana na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuleta ubingwa wa Ulaya ambapo, walibeba mabango yenye ujumbe wa kumshukuru.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo jana, Fulham ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Sheffield United kwenye Uwanja wa Bramall Lane.
Hadi mapumziko, Fulham ilikuwa ikiongoza 1-0 kwa bao lililofungwa na C. Porter dakika ya 31 kabla ya H. Rodallega kusawazisha dakika ya 75.

No comments: