Wednesday, 15 January 2014

waendeza bodaboda wakimbia maiti ya mwenzio

Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.

Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.

Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.

Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea mtafaruku mkubwa.

Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.

Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.

Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si waumini wa Kanisa lake.

Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.

Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.

Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.

No comments: