Sunday 26 January 2014

Essien atimkia Italia

KIUNGO, Michael Essien anahaha kutafuta njia za kulikimbia benchi Chelsea na sasa amemtuma wakala wake aende AC Milan kuomba nafasi ya kucheza timu hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Wakala wa staa huyo wa kimataifa wa Ghana, Fabian Piveteau kwa sasa yupo Italia kujadili namna ya kumpatia mteja wake nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Rossoneri ili kuweka hai nafasi yake ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil baadaye mwaka huu.

Essien amecheza mechi tano tu kwenye Ligi Kuu England msimu huu tangu aliporejea klabuni hapo na kocha Jose Mourinho mwaka jana. Ili kufanikiwa kujiondoa kwenye benchi, Essien anadhani Milan ni mahali pazuri zaidi kwenda.

Kwenye kikosi cha Chelsea, Essien alicheza kwa dakika zote 90 mara moja tu msimu huu wakati timu hiyo ilipomenyana na Crystal Palace, Desemba mwaka jana.

No comments: