CLARENCE Seedorf amebainisha kwamba atakuwa kocha mpya wa AC Milan baada ya kutangaza kustaafu soka.
Seedorf (37), aliyeichezea miamba hiyo katika ligi ya Serie A kuanzia 2002 mpaka 2012, atachukua nafasi ya Massimiliano Allegri, aliyefukuzwa kama kocha mkuu baada ya kuanza vibaya msimu.
"Ninastaafu soka baada ya miaka 22," alisema Seedorf, na kuongeza "Shabaha yangu ni kuwa na njozi tena."
Kwa mujibu wa BBC, Milan kwa sasa wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu ya Italia.
Seedorf, kiungo wa zamani wa Uholanzi, ameichezea Milan mechi 400, akiisaidia kunyakua kombe mara mbili la ligi ya Serie A na ubingwa mara mbili wa Ligi ya Mabingwa.
Alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu tatu tofauti Ajax mwaka 1995, Real Madrid (1998) na Milan (2003, 2007).
No comments:
Post a Comment