Friday, 25 April 2014

Sudan.Kusini:Wanasiasa 4 wazuiwa kusafiri

Wanasiasa wanne wakuu walioachiliwa na serikali ya Sudan Kusini, wamepokonywa hati zao za usafiri walipokuwa wanajiandaa kuondoka nchini humo kusafiri hadi mjini Nairobi Kenya.
Mke wa marehemu John Garanga, Rebecca Garang, ambaye anashikilia cheo cha juu katika chama cha SPLM , ameambia mwandishi wa BBC Robert Kiptoo kuwa serikali haikutoa sababu ya kuwapokonya
Wanasiasa wakuu waliokuwa wamezuiliwa

hati za usafiri wanasiasa hao.
Serikali ya Sudan Kusini iliwaachilia wanasiasa hao waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir Disemba mwaka jana.
Waziri wa sheria alisema kuwa serikali ilifutilia mbali kesi dhidi ya wanasiasa hao wanne wakuu waliotuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi ambayo yamesababisha vurugu za wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Wanne hao akiwemo aliyekuwa kiongozi wa chama cha SPLM, walikanusha madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi, na pia wamekanusha uhusiano wowote na mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini.
Kuachiliwa kwao imekuwa moja ya matakwa makubwa ya waasi wanaopambana na serikali na ambao wanadaiwa kuwaua mamia ya watu katika mji wa Bentiu kwa misingi ya ukabila.
Pagan Amum aliwahi kuwa mshirika mkubwa wa Rais Salva Kiir
Takriban watu milioni moja wamelazimika kutoroka makwao tangu vita kuzuka Disemba mwaka jana.
Waziri wa sheria Paulino Wanawilla alisema kesi hiyo imetupiliwa mbali kwa sababu ya kusaidia juhudi za amani na mapatano katika nchi hiyo ambayo imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wanne hao ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha (SPLM) Pagan Amum, aliyekuwa waziri wa usalama Oyai Deng Ajak, aliyekuwa waziri wa ulinzi Majak D'Agoot na aliyekuwa balozi wa nchi hiyo nchini Marekani Ezekiel Lol Gatkuoth.

No comments: