Monday, 21 April 2014

Rais wa Nigeria aitisha mkutano wa dharura

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
 
Mkutano huo hata hivyo hukushirikisha magavana kutoka chama cha upinzani ingawa baadhi yao wanawakilisha maeneo yaliyoathiriwa na ghasia za hivi karibuni.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amefanya mkutano wa dharura na maafisa wake wa juu wa usalama kufuatia mashambulizi mfululizo yaliyosababisha vifo na utekaji nyara wa zaidi ya wasichana 100 katika shule ya sekondari ya serikali.

Bw. Jonathan pia alikutana na baadhi ya magavana wa majimbo hapo Alhamis katika mji mkuu Abuja. Mkutano huo hata hivyo hukushirikisha magavana kutoka chama cha upinzani cha All Progressive Congress, ingawa baadhi yao wanawakilisha maeneo yaliyoathiriwa na ghasia za hivi karibuni.

Licha ya kutoshirikishwa kwenye mkutano huo, gavana wa jimbo la Akwa Ibom, Godswill Akpabio  aliwaambia waandishi wa habari kwamba  Wanigeria wote wanatakiwa kushirikiana kutatua tatizo  la ukosefu wa usalama nchini mwao.

No comments: