Tuesday 1 April 2014

waumini wauganda wamshukuru Rais wao

WANANCHI wa Uganda kutoka dini mbalimbali jana walikusanyika kwenye Uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa maombi maalum.
Mbali na maombi maalum, wananchi hao walitoa shukurani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia saini mswada wa sheria unaozuia mapenzi ya jinsia moja.
Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu waliwahimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi katika ibada hiyo maalum.
Hiyo ni mara ya kwanza viongozi wa dini mbalimbali nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa ibada maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo vya ushoga.
Kwa mujibu wa BBC, Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo, ambayo raia wengi wa Uganda wameipigia debe sana.
Ibada hiyo maalum imefanyika katika uwanja wa uhuru wa Kololo mjini Kampala, baada ya karibu mwezi mmoja na nusu tangu Rais Museveni kuiidhinisha.
Tangu Rais Museveni kuidhinisha sheria hiyo kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakimtaka kubadili msimamo wake, huku baadhi ya mataifa yakipunguza msaada kwa Uganda.
Hata hivyo, raia wengi wa Uganda walimsifu Rais Museveni kwa hatua yake

No comments: