''Rais wa Palestina Mahmoud Abbas lazima afutilie mbali mkataba wa amani kati yake na kundi la Hamas ikiwa anataka amani.''
Hii ndio kauli ya waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu kwa Palestina.Awali, Israel ilisitisha kwa muda mazungumzo ya amani na wapalestina, baada ya wapalestina kutia saani mkataba wa amani na wapiganaji wa Hamas.
Marekani kwa upande wake imelaani mkataba huo, lakini haiko tayari kutangaza kuwa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati yamekwisha na kwamba bado inafanya jitihada kuhamikisha kuwa mambo yako sawa.
Makundi ya Fatah na Hamas yalikubaliana Jumatano kubuni serikali ya Muungano na kuafanya uchaguzi miezi sita baadaye.
Kundi la Fatah limekuwa likilumbana na kundi la Hamas, tangu lishinde uchaguzi wa wabunge mwaka 2006, kuwaondoa wanajeshi wa rais Abbas na Fatah kutoka ukanda wa Gaza wakati wa ghasia mwaka 2007 na kubuni serikali mbadala.
Bwana Netanyahu aliambia shirika la utangazaji la uimgereza (BBC)kuwa Rais Abbas, anaweza tu kupata kitu kimoja, amani na Israel au mkataba na Hamas, hawezi kupata vyote.
Alisema kuwa Israel inaweza tu kurejelea mazungumzo ya amani na wapalestina wakati wataamua kufutilia mbali mkataba wa amani na Hamas ambao anasema ni chanzo cha ugaidi.
No comments:
Post a Comment