Wednesday, 16 April 2014

kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah kujulikana kabla ya kuelekea Brazil

Mjadala mkali umeibuka nchini Ghana kuhusu mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Kwesi Appiah, mkataba unaotarajiwa kutamatika ndani ya miezi michache ijayo.

Mjadala huu unakuja kufuatia kama ule ulioibuka mwaka 2010 ambapo chama cha soka nchini humo FA kilalalmikiwa kwa kushindwa kumuongezea mkataba mwingine aliyekuwa kocha mkuu wakati huo, Milovan Rajevac ambaye baadae alilazimika kuondoka.
Vyanzo vyakuaminika toka ndani ya chama cha soka nchini Ghana FA, zinasema kuwa mktaba wa kocha Appiah unatamatika tarehe 18 ya mwezi July mwaka huu.

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah akisimamia mazoezi ya timu yake
Reuters/Siphiwe Sibeko
Hata hivyo rais wa FA Kwesi Nyantakyi licha ya kuwepo kwa shinikizo la kutakiwa aweke bayana iwapo atamuongezea mkataba kocha huyo, amesema kutokana na mchango mkubwa wa Appiah chama hicho hakitakuwa na hiaya juu ya kumuongezea mkataba.
Nyantakyi ameongeza kuwa kocha Appiah ndiye aliyewezesha timu hiyo kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil, lakini hakuishia hapo tu akazifunga timu inayoshika nafasi ya sita na ya nne kwenye msimamo wa viwango vya soka duniani.
Licha ya kumwagia sifa kocha huyo, Kwesi anasema kuwa uamuzi wa mwisho utafanywa na kamati ya utendaji ya chama hicho ambapo wajumbe wataamua iwapo wamuongezee mkataba ama wasitishe na kutafuta kocha mwingine kabla ya kuelekea fainali za kombe la dunia.
Timu ya taifa ya Ghana iko katika kundi G pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani, Ureno na Marekani ambapo mchezo wake wa awali utapigwa tarehe 16 ya mwezi June dhidi ya Marekani kwenye uwanja wa Estadio das Dunas.

No comments: