Ili kufanya mgomo wenye ufanisi mkubwa,
rubani wa Ufaransa watasita kufanya kazi kwa masaa kadhaa kati ya Mei
tarehe 3 na Mei tarehe 30.
Kufuatia likizo ya mwisho wa wiki, usitisho mkubwa na uchelewsho wa safari za ndani na za nje unasubiriwa kutokana na mgomo wa rubani.
Kutokana na shria ya mwaka 2012, rubani wanatakiwa kutoa taarifa au kuwajulisha waajiri wao masaa 48 kabla ya kufanya mgomo. Sheria hiyo itawezesha ratiba nzuri ya safari na kuwaonya abiria ipasavyo iwapo kutakuwa na mgomo wa makampuni ya ndege.
Muungano wa French Pilot Union umesema kuwa sheria hiyo ya kutoa onyo masaa 48 kabla ya mgomo itawezesha makampuni ya ndege kuleta rubani kutoka nchi za nje na hivyo basi madhumuni ya mgomo wao kutochukuliwa ipasavyo.
Muungano huo ulieleza kuwa licha ya asilimia 85 ya rubani kufanya mgomo hivi karibuni, hakuwa na usitisho wala uchelewesho wowote wa ndege kutokana na makampuni ya ndege kuwaleta rubani hasa kutoka katika mashariki ya bara Ulaya.
No comments:
Post a Comment